Friday 21 March 2014

Masoud Kipanya:HAKUNA BIASHARA KUBWA ZAIDI YA KUZALISHA CHAKULA



 UKIWA MKULIMA UNAUWEZO WA KULISHA NA KUWA TAJIRI

 Masoud Kipanya akizungumza na wakulima


Mercy, Mwakilishi kutoka Shirika la ONE katika mazungumzo yake alisema kwamba tajiri mkubwa wa afrika anaitwa Dangote ni mkulima, maana yake nini? 

Maana yake Dangote sio kwamba analima hewani ila anafanya taratibu zote kama sisi tunavyofanya.  Yeye anaishi Nijeria, ardhi iliyopo huko ni sawa na iliyopo Tanzania tena inawezekana Tanzania ikawa na maeneo mazuri zaidi. 

Sisi kama binaadamu tunaweza kua mabilioni, kwa sababu binaadamu anaweza kuacha vitu vyote lakini chakula ni lazima ale, sasa kuna biashara kubwa zaidi ya kuzalisha chakula? Hakuna.
Ukiwa mkulima unanfasi kubwa ya kulisha jamii lakini vile vile na kutajirika. 
 Kipanya akisisitiza umuhimu wa kilimo

Mimi kama Masoud Kipanya nina miradi miwili ambayo ninaifanya.Wa kwanza ni Maisha plus-kipindi cha televishen sasa hivi tunawaganisha vijana pamoja na wakina mama wazalishaji wa chakula. Nia yetu kubwa ni kuwaambukiza hawa vijana ili hii tabia ya kutoroka kutoka vijijini kukimbilia mijini iweze kuisha, watu waweze kujua namna wanavyoweza kutembea juu ya hela wakiwa kijijini .

Mradi wa pili tunaufanya na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, ambapo tuna vijana 100 tumewaweka porini kwa kufuata model ileile ya maisha plus. Wale vijana 100 tumeanza kukaa nao tangu mwaka jana (2013) mwezi 4 na wanafanya kilimo cha hali ya juu kabisa. Hata mimi mwenyewe mjini nimeanza kuhama kabisa utanikiuta Tabora. Dar es salam tunaacha AC, magari mazuri kwa sababu tunajua tunakoelekea.


Mwaka huu vijana wamelima hekta 20 za tumbaku lakini vile vile wanalima na mahindi. Mwakani wanatarajia kulima hekta 100 kwa hivyo kuna unawezekano wa kutengeneza milioni 700 au 800 ni mkubwa sana. Sasa unasemaje kuhusu kilimo?

Masoud Kipanya akiwa na mabalozi wenzake, Profesa J na Mrisho Mpoto











No comments:

Post a Comment