Thursday 3 April 2014

FREDRICK KARIA: NINA NDOTO ZA KULISHA TANZANIA NZIMA


"NIA YANGU NI KUIFANYA TANZANIA GHALA LA CHAKULA"


Fredric Karia ni Mkulima. Anafanya kilimo cha nyanya, mpunga na mahindi. Mbali na kufamya kilimo pia ni Mukurugenzi wa kampuni binasfi Kicharugu Logistic Limited. Fredrick ni mtaamu wa mambo ya usalama wa majini na mazingira (Maritarime Safety and Environment Management)

Swali: Nini kilikusukuma ukaamua kufanya kilimo?

Fredrick:  Kwanza nilikataa kuwa maskini, nilifanya kila njia kutimiza malengo yangu.  
Wazo la Kulisha Tanzania nzima, sikuona sababu ya  watu wa nje kuja nchini kutusaidia  wakati tuna ardhi nzuri na yenye rutuba. Nia yangu ni kuifanya Tanzania ghala kuu la chakula, akitokea mtu mwingine mwenye mawazo kama yangu basi Tanzania ile dhana ya “Kilimo Kwanza” itakua kweli


Fredrick: nilianza kulima si muda mrefu, ni mwaka jana 2013 hadi sasa. 
Nalima Mpunga na nyanya

Swali: ni mafanikio yapi uliyoyapata kutokana na kilimo?



Mafanikio yapo. Nina eneo (ardhi) hekari 35 Dar es Salaam, hekari 3.5 Dododma, 3.5 Mlandizi  na Kiluvya. 
Pia nimewekeza kwenye viwanja








Swali: Unawezaje kufanya shuguri za kilimo wakati muda mwingi unakua safarini au kwenye majukumu mengine?

Rafiki wa Fredrick, akiandaa shamba


"Nikiwepo hua nafanya mwenyewe ila ninaposafari wanakuwepo wafanyakazi wangu wa shamba. Kwa mfano sasa hivi sipo nchini shughuri za shamba zipo chini ya rafiki yangu. Huwa namkabidhi vitu vyote na mahitaji yote"

Shughuri zangu za shamba zinakwenda vizuri na mambo yote yapo kwenye taratibu nzuri ili kuhakikisha kilimo kinakua. 







Swali: Changamoto zipi unakumbana nazo?



Zipo changamoto nyingi kwa kweli unaweza ukalima mwisho wa msimu ukitarajia kupata gunia 100 ukaanguka, na umetumia pesa nyingi tayari, pesa ikiwa ya mkopo ndio hasara zaidi.

  







"Pia changamoto niliyonayo trekta la kukodi, "natumia gharama kubwa sana" 

Changamoto nyingine ni wadudu wakishambulia mazao wanasababisha hasara kubwa hivyo umakini unahitajika hasa katika kufata taratibu za "kilimo cha kisasa"




Naungana na ANSAF kwenye kapeni ya "KILIMO INALIPA, JIKITE" kuwakumbusha viongozi wa Afrika kutenga asilimia 10 ya bajeti kwenye kilimo ili kuleta uzalishaji wenye tija.



Niliamua kulima mpunga baada ya kuona mchele ukitumika sana kwa chakula kwa watanzania walio wengi.

Napenda kuwaambia vijana wenzangu wasitegemee kuajiriwa peke yake kwani wanaweza kujiajiri wenyewe kupitia sekta hii ya kilimo.

ANSAF kupitia kapeni ya Kilimo Inalipa Jikite ina lengo la kuwasaidia wakulima wadogo ili kuondokana na lindi la umaskini.